Kama umekuwa ukijiuliza swali moja kati ya haya basi umefikia sehemu sahihi!
Nataka kujiunga whatsapp.
Jinsi ya kudownload Whatsapp
Jisajili Whatsapp kiswahili

Je! Unataka kujiunga Whatsapp na haujui ni namna gani unaweza kujisajili? Basi kuwa pamoja nami hadi mwisho wa post hii utoke ukiwa mtaalamu wa kuwaunganishia Whatsapp washikaji kwenye simu Zao!.
Takwimu kutoka kwenye blogu ya Statistics zinaonesha kwamba watumiaji wa whatsapp wamefika takribani Milioni 1600 mnamo mwanzoni mwa mwaka 2017.
![]() |
Takwimu zikionesha idadi ya watumiaji hai( Active users) wa Whatsapp kila mwezi |
Jinsi Ya Kujiunga Whatsapp.
Kujisajili Whatsapp sio kazi kubwa wala kazi ngumu sana kama watu wengi walivyoaminishwa.
Ni kitendo kinachochukua hatua chache ambazo ni rahisi kuzifuata kama jinsi nilivyojitahidi kukufafanulia na kuzirahisisha zaidi hapa Chini ili kumuwezesha kila mmoja wetu mwenye uhitaji wa kujiunga na kuanza kufurahia ulimwengu wa kuchati, kutumiana picha, videos, animations na taarifa mbalimbali za mipasho kupitia Whatsapp kwenye simu yake hasa ya Android, Windows au iPhone ( Hizi ni aina za simu ambazo Watanzania wengi tunazitumia ).
Hatua Za Kufuata Ili Kujiunga Na Whatsapp
- kwanza hakikisha simu yako ina chaji na upo sehemu yenye mtandao mzuri.
- Kifurushi cha MB's kwenye simu yako ni jambo ambalo si la kusahau.
1. Kudownload Whatsapp ( Kupakua whatsapp )
Jinsi ya kudownload Whatsapp.
1. Kwenye simu yako, ingia kwenye application iliyoandikwa "Playstore"
2. Baada ya playstore kufunguka, search neno ''WhatsApp".
Hapo utapata results nyingi lakini bonyeza ile iliyoandikwa "Whatsapp Messenger" kisha,
3. Bonyeza "install" Utaona application inaanza kujidownload na ikiisha itakuandikia installing whatsapp messenger.
Baada ya hapo, application ya whatsapp ataanza kuonekana kwenye Home ya simu yako.
4. Bonyeza "Open" kufungua WhatsApp na kuanza kujisajili/ kujiunga kama nilivyoelezea kwenye hatua ya pili hapa chini
2. Kujisajili Whatsapp
Kujisajili whatsapp unatakiwa kufuata hatua zifuatazo.
1. Hatua ya kwanza ni kukubali Terms and Conditions za WhatsApp kwa kubonyeza "Agree and Continue"
2. Hatua ya pili ni kubonyeza "continue" endapo utapata option kama hii ya kukuomba ruhusa ya kuzi-access namba za marafiki, videos, na picha zalizopo kwenye simu yako
* Usisahau kubadilisha jina la nchi! mahali ilipoandikwa "United States" inabidi uweke Tanzania na jinsi ya kubadilisha ni rahisi tuu, bonyeza jina la United States kisha uchague Tanzania.
* Baada ya kuchagua Tanzania, utaona namba ya hapo mwanzo itabadilika pia.
- Hiyo moja itatoka na itakuja +255 ambayo huwa ipo badala ya " 0 " ya mwanzoni mwa namba za simu
4. WhatsApp itataka kutuma sms ya uthibitisho kwenye namba ya simu uliyioweka.( hapa unaweza kutumia namba nyingine kutumiwa hizo Verification codes )
6. Tarakimu sita zitatumwa na utazijaza kwenye nafasi kama hii inayoonekana kwa hapa chini.
* Kama namba uliyoijaza ipo kwenye simu unayoitumia kujiunga na Whatsaap basi hautakuwa na haja ya kuziingiza hizo namba za uthibitisho zilizotumwa kwa sababu Whatsapp ina uwezo wa kuziingiza automatic.
6. Hatua ya mwisho katika kujisajili WhatsApp ni kujaza kitufe kama kinavyoonekana hapa chini kisha malizia kwa kubonyeza "Done"
Yey! Kazi yetu ya kudownload, kijisajili, na kujiunga na WhatsApp imefikia kikomo. Sasa unaweza kuanza kutumia na kuufurahia ulimwengu wa Whatsapp.
Kwa maelezo na hatua za hapo juu, ni imani yangu kwamba hakuna tatizo utakalo kumbana nalo.
Kama lipo, basi
Kuwa huru kuuliza swali Lolote Ndugu yangu! Tupia Comment yako hapa Chini nami nitakuwa Chonjo kukujibu
Kuwa pamoja nami kwa kuitembelea blogu hii mara kwa mara ili tubadilishane maarifa na upate kujifunza ujanja wa Simu, WhatsApp, Facebook, Instagram, Blogging, Ujasiriamali wenye Tija, Habari pamoja na videos za vichekesho ili kuifanya siku yako kuwa Murua!.
Tafadhali, Share post hii....Na Siku Tukikutana....Unikumbushe nikununulie Soda / bia!
Tukutane kwenye post inayofuata na usisahau kulike page & subscribe youtube channel.